Pata Kisima na Bwawa bora kwa gharama nafuu na kwa kujali thamani halisi ya pesa yako

Hon. Jumaa Aweso (MP) Deputy Minister Ministry of Water and Irrigation arrive at DDCA

Posted on: November 23rd, 2017

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameitaka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na wananchi kwa ujumla kuwatumia Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) ipasavyo ili  kuleta maendeleo kwenye Sekta za Maji na Umwagiliaji nchini kutokana na uwezo mkubwa ilionao. Hayo ameyasema wakati akiongea na wafanyakazi wa DDCA wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika taasisi hiyo kwa lengo la kujionea utendaji na changamoto zao za kikazi, na jinsi ya kuiongezea uwezo taasisi hiyo katika kufanikisha utimizaji wa majukumu yake kwa ufanisi. ‘‘Tumekua tukilalamika kuhusu utendaji mbovu wa makampuni mengi, ambayo yamekuwa yakilipwa fedha nyingi bila kukamilisha miradi ya visima na mabwawa na kuigombanisha Serikali na wananchi wake. Wakati tuna DDCA ambao wana uwezo mkubwa na wamekuwa wakifanya kazi nzuri,’’ alisema Aweso. ‘‘Umefika wakati wa kuwatumia DDCA kwenye kazi zetu za uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa, hawa kwa kiasi kikubwa watakuwa mwarobaini wa changamoto za maji kwa maeneo ambayo wananchi wake wana kilio cha huduma ya majisafi na salama, na kama wizara tutawajengea uwezo ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi’’ alisisitiza Aweso.