Pata Kisima na Bwawa bora kwa gharama nafuu na kwa kujali thamani halisi ya pesa yako

KM - MoWI Prof. Kitila Mkumbo akiongea na DDCA Menejimenti

Posted on: September 7th, 2018

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akiwa pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) kwenye kikao cha pamoja kujadili utendaji wa Wakala pamoja na kutafuta ufumbuzi wa  changamoto zinazoikabili wakala. Katika kikao hicho Katibu mkuu alitolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu utendaji wa wakala pamoja na kutoa maelekezo kwa watendaji wa wakala kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili wakala usonge mbele.